rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Maandamano nchini Iraq: Takwimu rasmi za watu waliouawa ni 157, pamoja na 111 Baghdad
  • Machafuko Chile: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 15 baada ya watu watatu kuuawa (serikali)
  • Rais wa Chile Piñera ajaribu kutuliza hasira za waandamanaji baada ya maandamano mapya

WHO DRC Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

WHO kuanza kutoa chanjo ya dharura ya surua nchini DRC

media
Chanjo ya surua AFP

Shirika la afya duniani WHO limesema litaanza kutoa chanjo ya dharura kukabiliana na ugonjwa wa surua miongoni hasa mwa watoto katika mikoa sita, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.


WHO inasema ugonjwa huo umesababisha vifo vya watoto 3,600 tangu kuanza mapema mwaka 2019.

“DRC inakabiliwa na hali hii kwa sababu watoto wengi, hawapati chanjo ya mara kwa mara,” amesema Deo Nshimirimana mwakilishi wa WHO.

Ripoti zinaeleza kuwa kuna kesi 183,000 ya maambukizi ya ugonjwa huo, tangu tarehe 17 mwezi Septemba.

Idadi ya watu walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo, ni wengi ikilinganishwa na wale waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Aidha, WHO imesema kuwa, watoto 825,000 watapata chanjo hiyo katika majimbo 24 nchini humo kwa kipindi cha siku tisa zijazo.