rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Zimbabwe Robert Mugabe

Imechapishwa • Imehaririwa

The Herald: Saratani ndio iliyomuua Mugabe

media
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa uhai wake, wakati huo alitangaza kwamba hatakipigia kura chama cha Zanu-PF Julai 29, 2018. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe, alikuwa anasumbuliwa na saratani, iliyosababisha kifo, mapema mwezi huu nchini Singapore.


Gazeti linalofadhiliwa na serikali nchini humo The Herald, limeripoti kuwa licha ya Mugabe kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu, afya yake ilianza kuwa mbaya baada ya kuondolewa madarakani na jeshi mwaka 2017.

Wakati wa uhai wake, Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 alikuwa anakwenda mara kwa mara kupata matibabu nchini Singapore wakati huo, ikishukiwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na saratani ya tezi dume.

Rais Emmerson Mnangagwa akiwa jijini New York amenukuliwa na Gazeti la The Herald akiwaambia wafausi wa chama cha ZANU PF kuwa, madaktari walishindwa kuendelea kumpa matibabu Mugabe kwa sababu ya umri wake mkubwa lakini pia saratani ilikuwa imesambaa sana mwili na hivyo, matibabu yalikuwa hayasaidii.

Mugabe aliyeongoza nchi hiyo kwa miaka 37, anatarajiwa kuzikwa mwezi ujao katika makaburi ya mashujaa jijini Harare.