Pata taarifa kuu
MISRI-HARAKATI-SIASA

Mwanasheria maarufu akamatwa nchini Misri

Malaka nchini Misri zinamshikilia Mwanasheria Mshindi wa tuzo ya Haki za Binadamu baada ya kufuatilia uchunguzi wa kukamatwa kwa waandamaji waliokuwa wakimpinga Rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi.

Rais wa Misri  Abdel Fattah al-Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Tarek al-Awadi Mwanasheria wa Mahienour El-Massry anasema mwanasheria huyu alikamatwa muda mfupi tu baada ya kuondoka katika ofisi ya mwendesha mashataka wa serikali jijini Cairo alipokuwa akifuatiliwa kukamatwa kwa waandamaji.

Mamia ya Wamisri waliingia Mitaani jijini Cairo pamoja na miji mingine wakishinikiza kuondoka madarakani kwa Rais al-Sisi.

Kwa Mujibu wa kituo kinachoshughulikia haki za kiuchumi na kijamii nchini humo Watu 365 wamekamatwa kutokana na Maaandamano hayo

Mwezi wa Decemba 2013, kufuatia Jeshi kumpindua rais  wa zamani Mohamed Morsi baada ya maandamano ya kushinikiza ang'atuke Madarakani Bi El-Massry alikamatwa na kufungwa Jela hadi Septemba 2014 kwa kosa la kushiriki maandamano bila kibali akiwa Gerezani ndipo alipata tuzo ya haki za binadamu

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.