Ufaransa kusaidia Sudan kuondolewa katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi
Waziri wa Mambo ya nje wa ufaransa Jean-Yves Le Drian akiwa jijini Khartounm nchini Sudan amesema nchi yake itaendelea kuweka shinikizo ili Sudani iondolewe katika nchi ambazo zimeorodheshwa na Marekani, kuwa zinafadhili ugaidi.
Imechapishwa:
Le Drian amekuwa nchini Sudani na kuwa kiongozi wa juu wa Ufaransa kuzuru taifa hilo baada ya miaka 10, na ziara hii imekuja, baada ya mabadiliko ya uongozi nchini Sudani.
Hivi karibuni Waziri Mkuu Abdallah Hamdok alifanikiwa kuunda serikali ambayo inajumuisha raia wa kawaida na jeshi.
Hayo yamekuja baada ya jeshi na viongozi wa maandamano kuafikiana kuhusu suala la kugawana madaraka.
Maelfu ya raia waliuawa katika maandamano ya kumng'atua madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Omar Hassan Al Bashir ambaye kwa sasa anakabiliwa na mkono wa sheria.