Pata taarifa kuu
DRC-UBELGIJI-USHIRIKIANO

DRC na Ubelgiji zatia saini kwenye Itifaki za Mkataba wakati wa ziara ya Rais Tshisekedi Brussels

Ziara ya serikali ya Felix Tshisekedi nchini Ubelgiji inaendelea. Jumanne wiki hii rais wa DRC amepokelewa kwa heshima ya kijeshi na Waziri Mkuu Charles Michel.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi akiwa na Mfalme wa Ubelgiji, Mfalme Philippe, kwenye kasri ya kifalme, Brussels Septemba 17, 2019.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi akiwa na Mfalme wa Ubelgiji, Mfalme Philippe, kwenye kasri ya kifalme, Brussels Septemba 17, 2019. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zimesaini nakala kadhaa za ishara kwa kuanzishwa tena ushirikiano kabla ya Rais Tshisekedi kupokelewa na Mfalme wa Ubelgiji.

Ni ziara yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya DRC na Ubelgiji. Kuna nia kwa pande zote kuonyesha kuwa ukurasa mpya umefunuliwa, wakati miaka ya hivi karibuni katika utawala wa Joseph Kabila, nchi hizo mbili zilikuwa kwenye malumbano ya kidiplomasia.

Kinshasa iliwafukuza maafisa wa Ubelgiji na kusitsha ushirikiano wa kijeshi. Balozi ndogo za Ubelgiji nchini DRC zilifungwa na Ubelgiji iliamua kubana msaada wake kwa serikali na kuuelekeza kwa vyama vya kiraia.

Umoja wa Ulaya ulifanya vivyo hivyo, lakini haikusema wazi.

Ziara ya rais Felix Tshisekedi nchini Ubelgiji ni ishara ya kuanza upya kwa uhusiano baina ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ubelgiji, baada ya kutetereka katika dakika za mwisho za utawala wa rais Joseph Kabila.

Ikulu ya Kinshasa inasema huu ni ukurasa mpya uliofunguliwa, upande wa Ubelgiji wanasema hii ni ziara yenye ishara nzuri ambapo Ubelgiji inafurahishwa na hatua hiyo ya felix Tshisekedi kuzuru kwanza Brussels, Kabla ya Paris katika ziara yake hiyo ya kwanza barani Ulaya, ambapo mwanadiplomasia mmoja wa Ubelgiji amesikika akisema kwamba huu ni udhibitisho wa kudumisha uhusiano wa mataifa hayo mawili.

Hata hivyo baada ya ziara ya mjumbe na maafisa wa Ubelgiji mwezi Mei mwaka huu, hakuna hatua chanya iliopigwa katika uhusiano baina ya pande hizo mbili. Kile kinachotarajiwa kusainiwa hii leo Jumanne tayari kimekwisha jadiliwa, jumla ni mikataba minne ya makubaliano, pamoja na barua inayoashiria kurejea kwa mahusiano kati ya Kinshasa na Brussels.

Inatarajiwa kuona uhusiano wa kijeshi uliositishwa wakati wa utawala wa rais Joseph Kabila ukirejea, kufunguliwa upya kwa ubalozi mdogo wa Congo katika mji wa Anvers na kurejeshwa kwa shguhuli katika ubalozi mdogo wa Ubelgiji jijini Lubumbashi uliofungwa wakati wa mvutano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.