rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

DRC Ebola WHO

Imechapishwa • Imehaririwa

Waziri wa zamani wa afya nchini DRC Oly Ilunga akamatwa

media
Waziri wa zamani wa afya nchini DRC Oly Ilunga FABRICE COFFRINI / AFP

Waziri wa zamani wa Afya nchini DRC Oly Ilunga ambaye amekuwa akituhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya pesa zilizotolewa kukabiliana na uginjwa wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo, ametiwa nguvuni siku ya Jumamosi jijini Kinshasa, kesi nyingine tatu za maambukizi mapya zikiripotiwa.

 


Msemaji wa polisi jijini Kinshasa Kanali Pierrot Rombaut Mwanamputu amesema Dakatari Ilunga amewekwa chini ya Ulinzi katika kituo cha polisi na atafikishwa Mahakamani siku ya Jumatatu wiki ijayo.

Dokta Oly Ilunga anatuhumiwa kutumia vibaya fedha zilizotolewa na serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo kukabiliana na virusi vya Ebola ambapo baadaye alijiuzulu wadhifa wake katika kile alichodai kutokubaliana na majaribio ya chanjo ya pili ya Ebola.

Wakati hayo yakiarifiwa, kesi mpya tatu za Ebola zimethibitishwa kwa mujibu wa taarifa iliotolewa siku ya Ijumaa na shirika la Afya Duniani WHO.

WHO imesema kesi mbili zimeripotiwa huko Mambasa katika jimbo la Ituri na Beni Mashariki mwa nchi hiyo.

Eneo la kiafya la Kalunguta mjini Beni mkoa wa Kivu Kaskazini pamoja na Mandima na Mambasa katika Mkoa wa Ituri ndiyo yaliyoathiriwa zaidi na Ebola.

Mbali na hayo, takwimu zinaonyesha kuwa kuanzia Septemba tarehe 9, kesi 281 zilizoshukiwa kuwa za Ebola 59 zilithibitishwa na kuwekwa katika vituo 15 vilivyotengwa kutoa huduma ya Ebola.

Kwa jumla tangu kuripotiwa kwa maradhi hayo mwaka mmoja uliopita, watu 2,71 wamepoteza mzaisha na zaidi ya 3,084 kuambukizwa.