Pata taarifa kuu
BURUNDI-UFARANSA-HAKI

Waziri wa zamani wa Burundi aombwa kufungwa miaka 3 Jela

Mahakama ya Nanterre, nchini Ufaransa imesikiliza kesi ya waziri wa zamani wa Burundi, ambaye pia afisa wa zamani wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto Unesco na mkewe.

Kesi hiyo imesikilizwa katika mahakama ya Nanterre, Jumatatu, Septemba 9. (Picha ya kumbukumbu).
Kesi hiyo imesikilizwa katika mahakama ya Nanterre, Jumatatu, Septemba 9. (Picha ya kumbukumbu). JACK GUEZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wanashtumiwa usafirishaji haramu wa binadamu. Ofisi ya mashitaka jijini Nanterre inawashtumu wawili hao kumnyanyasa raia wa Burundi kwa miaka kumi kwenye makaazi yao, magharibi mwa Paris.

"Methode, hapa tuko uso kwa uso, sikuwahi kukuomba upige magoti mbele yangu, kamwe," amesema Gabriel Mpozagara kwa sauti kali. "Hauwezi kumfanyia vitisho mlalamikaji," jaji amesema. "Usitumie sauti hiyo, usimtishi mtu hapa, " jaji ameongeza. Mpaka kesi hii kuanza kusikilizwa, mwendesha mashtaka wa zamani na Waziri wa zamani wa Sheria wa Burundi Gabriel Mpozagara alijaribu, kwa sauti ndogo kutetea maneno hayo, bila hata hivyo kufaulu.

Methode Sindayigaya ambaye alifanyiwa madhila hayo, alikuja nchini Ufaransa akiandamana na mwanae, huku akibaini kwamba allijaribu kuwaambia wanadoa hao kuwa alipoteza pasipoti yake. Gabriel Mpozagara na mkewe wamesema kuwa hawakutaka kumuachilia yende hovyo mitaani. Alikuwa kama "mtoto wa nyumbani, rafiki ambaye wakati mwingine alisaidia na kazi za nyumbani". Alitaka kubaki katika makazi yangu, amesema Gabriel Mpozagara.

Kesi hiyo ilisikilizwa Jumatatu wiki hii.

"Kufikia hatua ya kutomuona mke wake na watoto wowote kwa miaka kumi? " jaji amemuuliza mke wa Mpozagara. "Alikuwa huru kama hewa, ni kosa lake, kwani hakutaka kuondoka," amejibu mkee wa Mpozagara.

"Leo, niko huru"

Methode Sindayigaya ameileza mahakama jinsi, alitumiwa kuhudumia watoto kwa miezi mitatu. Miaka kumi alifanya kazi saa 19 kati ya 24, kulishwa vibaya, makazi duni, na kadhalika, wanasheria wake wamesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.