Imechapishwa • Imehaririwa
Waziri Mkuu wa Algeria kuachia ngazi kwa ajili ya uchaguzi

Waziri Mkuu wa Algeria Noureddine Bedoui atajiuzulu hivi karibuni, ili kutoa nafasi ya kuwepo kwa Uchaguzi Mku mwaka huu.
Ripoti zinasema kuwa, uamuzi huo umefikiwa kutokana na maandamano dhidi ya serikali ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa sasa.
Waandamanaji wanamtaka Waziri Mkuu huyo kuondoka madarakani, kama ilivyokuwa kwa rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika aliyelazimiwa kujiuzulu mwezi Aprili.
Waandamanaji pia wanataka mabadiliko katika mfumo wa uongozi wa nchini humo.