Pata taarifa kuu
NIGERIA-AFRIKA KUSINI-USALAMA

Chuki dhidi ya wageni Afrika Kusini: Nigeria yarudisha nyumbani raia wake 600

Serikali ya Nigeria imetangaza kuruwarudisha nyumbani raia wake 600 kuanzia Jumatano, 11 Septemba. Uamuzi huo umechukuliwa na shirika la ndege la Air Peace kutoka Nigeria na kuungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.

Shirika la ndege la Air Peace litaanza zoezi la kuwarudisha nyumbani raia wa Nigeria Jumatano hii 11 Septemba.
Shirika la ndege la Air Peace litaanza zoezi la kuwarudisha nyumbani raia wa Nigeria Jumatano hii 11 Septemba. © Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Katika kuunga mkono waathiriwa wa ghasia zinazochochewa na chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini, Allen Onyema, mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air Peace, amekubali kuwasafrisha kwa bure raia wa Nigeria wanaotaka kurudi nyumbani kufuatia hali hiyo inayoendelea nchini Afrika Kisini.

Kuanzia Jumatano wiki iliyopita, watu 600 kwa jumla ya watu 100,000 kutoka Nigeria wanaoishi nchini Afrika Kusini, wamejiorodhesha kurudi nyumbani kwa hiari yao, kwa mujibu wa vyanzo kutoka ubalozi wa Nigeria Johannesburg.

Zoezi hilo lilitarajiwa kuanza Ijumaa ya wiki iliyopita, lakini lilicheleweshwa kwa sababu za kiutawala. Wahamiaji kutoka Nigeria walitakiwa kwanza kupata cheti cha kusafiri kwa sababu wengi wao hawana pasipoti halali. Tatizo hilo limepatiwa suluhu, kwa mujibu wa vyanzo hivyo. Zoezi la kuwarudisha nyumbani litaanza Jumatano hii, Septemba 11, serikali ya Nigeria imesem akatika taarifa. Ndege ya kwanza ya shirika la ndege la Air Peace itasafiri na abiria 320. Na nyingine itashiriki zoezi hilo hivi karibuni.

Hatua hiyo inakuja wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeanza kuwa mzuri, baada ya kukumbwa hali ya sintofahamu kwa wiki moja iliyopita . Baada ya mvutano wa siku kadhaa, Abuja ilimtuma mjumbe wake kwenda Afrika Kusini na ikasema kwamba inataka kutafuta suluhisho na Pretoria. Na wakuu wa nchi hizi mbili wanatarajia kukutana mapema mwezi Oktoba nchini Afrika Kusini.

Mvutano kati ya nchi hizi mbili zenye nguvu kiuchumi barani Afrika unaweza kusababisha athari kubwa. Wiki iliyopita, Nigeria ilisusia Mkutano wa Uchumi wa Dunia uliofanyika jijini Cap, nchini Afrika Kusini.

Mtu mwengine aliuawa Johannesburg, mwishoni mwa wiki hii iliyopita na kufikia 12 idadi ya watu kutoka nchi za kigeni ambao wameuawa katika ghasia zinazochochewa na chuki dhidi ya wageni zilizozuka tangu wiki iliyopita nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.