Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Raia DRC wasubiri kuona upinzani unashiriki au la vikao vya Bunge

Wanasiasa wa Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanatarajia kukutana hii leo alhamisi kuamua iwapo watashiriki au la katika vikao maalum vya bunge jijini Kinshasa kuandaa sherehe za kutawazwa rasmi baraza la serikali lililoteuliwa hivi karibuni.

Moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. JUNIOR D.KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanatarajia kukutana hii leo alhamisi kuamua iwapo watashiriki ai la katika vikao maalum vya bunge jijini Kinshasa kuandaa sherehe za kutawazwa rasmi baraza la serikali lililoteuliwa hivi karibuni.

Upinzani umepinga Mpango Kazi wa serikali hiyo kama ulivyotolewa hivi majuzi na Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba, kufuatia kile unachosema hauna mashiko, wala hakuna kinachoaminiwa katika mpango huo.

Kauli hii imeungwa mkono na baadhi ya wabunge wa upande wa utawala, kwa mujibu wa Juvenal Munubo Mubi mmoja wa wabunge wa bunge la taifa wa chama cha UNC kinachoongozwa na Vital Kamerhe.

Ulinzi wa taifa hilo kubwa na tajiri lakini pia usalama, ni miongoni mwa mambo muhimu Sylvestre Ilunga Ilunkamba aliyoonyesha kuwa ni kipaombele cha serikali yake, huku akisema kuwa lengo la serikali yake ni kuhakikisha mamlaka ya serikali, inarejeshwa haswa kupitia maridhiano ya kitaifa.

Katika neno lake la ufumbuzi Waziri Sylvestre Ilunga alisema kuwa serikali yake itahakikisha masilahi ya wananchi yanapewa kipaumbele.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.