Pata taarifa kuu
SUDANI-SIASA-USALAMA

Hamdok kutangaza baraza lake la mawaziri ndani ya saa 48 zijazo

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, anatarajiwa kutangaza baraza lake la Mawaziri ndani ya saa 48 zijazo, miezi michache baada ya jeshi na viongozi wa maandamano kufikia mkataba wa kihistoria wa kugawana madaraka.

Waziri Mkuu Abdallah Hamdok alitawazwa Agosti 21, Khartoum, Sudani.
Waziri Mkuu Abdallah Hamdok alitawazwa Agosti 21, Khartoum, Sudani. Ebrahim HAMID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Sudan wamekuwa wakisubiri serikali mpya, tangu kuunda kwa baraza la serikali ya mpiti mwezi uliopita.

Shirika la habari la Sudan SUNA jana liliripoti kuwa, Waziri Mkuu Abdallah Hamdok anatazamia kutangaza baraza kamili la mawaziri siku mbili zijazo.

Hata hivyo awali shirika hilo lilibaini kwamba tayari Waziri Mkuu wa Sudan amewaidhinisha mawaziri 14 wa baraza lake la mawaziri; ambao ni wa kwanza kuteuliwa tangu kupinduliwa utawala wa muda mrefu wa rais wa nchi hiyo Omar al Bashir mwezi Aprili mwaka huu

Kutajwa kwa Baraza kulichelweshwa kwa sababu ya kuendelea kwa mashauriano na wadau mbalimbali ili kuunda serikali itakayokubaliwa na wote.

Serikali ya mpito ya Sudan itafanya kazi chini ya usimamizi wa Baraza la Utawala wa Mpito litakaongozwa na wajumbe 11 wakiwemo sita wa kiraia na wanajeshi watano; na litaongoza kwa muda wa miaka 3 kuelekea uchaguzi mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.