Pata taarifa kuu
CONGO-UFARANSA-USHIRIKIANO

Drian amuomba Rais Sassou-Nguesso kuchukua hatua kwa kiongozi wa upinzani Mokoko

Rais wa Congo Denis Sassou-Nguesso amepokelewa Jumanne, Septemba 3 katika ikulu ya Elysee kwa chakula cha mchana na Rais Macron. Mazungumzo yao yaligubikwa na suala la mazingira na uchumi.

Emmanuel Macron akimpokea Denis Sassou-Nguesso Élysée Septemba 3, 2019.
Emmanuel Macron akimpokea Denis Sassou-Nguesso Élysée Septemba 3, 2019. © ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya mkutano huo, rais wa Congo alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian na walizungumzia masuala nyeti hususan hali ya kisiasa nchini Congo.

Waziri Jean-Yves Le Drian amebaini kwamba amemuomba rais wa Congo kuchukuwa "hatua" kwa mwanasiasa wa upinzani Jean-Marie Michel Mokoko na watu wengine wanaofungwa.

Bw Drian amesema : nilimwambia nikisisitiza kuhusu suala hilo"

"Maneno haya ya Jean-Yves Le Drian yamepokelewa shingo upande na ujumbe wa Congo.

Jean-Claude Gakosso, Waziri wa Mambo ya nje wa Congo amesema: "Maneno haya nimeyapokea jinsi yalivyo. Lakini namfahamu vizuri Jean-Yves Le Drian na ninaweza kuthibitisha urafiki alio nao kwa Rais Sassou. Ni marafiki, kwa hiyo wanaweza kuongea mambo mengi.

Akiulizwa iwapo kuachiliwa kwa haraka kwa mpinzani Jean-Marie Michel Mokoko, anayezuiliwa kwa miaka mitatu sasa, inawezekana kwa upande wa rais Sassou, Waziri wa Mambo ya Nje aw congo amejibu akisema: "sijui, ni swali ngumu, nisingependa kutoa maoni yoyote, kwani suala hili liko mikononi mwa vyombo vya sheria ambavyo ninaheshimu. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.