Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

DRC: Waziri Mkuu atangazia Mpango Kazi wa serikali yake mbele ya wabunge

Waziri mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Sylvestre Ilunga Ilunkamba jumanne wiki hii amelihutubia bunge la kitaifa ambapo ametangazia Mpango Kazi wa serikali yake katika kulijenga taifa hilo, siku chache baada ya baraza la mawaziri kuteuliwa.

Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga ametangazai Mpango Kazi wa serikali yake mbele ya Bunge la kitaifa, Kinshasa (Septemba 3).
Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga ametangazai Mpango Kazi wa serikali yake mbele ya Bunge la kitaifa, Kinshasa (Septemba 3). © P. Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Ulinzi wa taifa hilo kubwa na tajiri lakini pia usalama, ni miongoni mwa mambo muhimu aliyoonyesha kuwa ni kipaombele cha serikali yake, huku akisema kuwa lengo la serikali yake ni kuhakikisha mamlaka ya serikali, inarejeshwa haswa kupitia maridhiano ya kitaifa.

Katika neno lake la ufumbuzi Waziri Sylvestre Ilunga amesema kuwa serikali yake itahakikisha masilahi ya wananchi yanapewa kipaumbele.

Hata hivyo wabunge wa upinzani wamesema wameshangazwa kuona hakuna takwimu zozote zilizotolewa, wala mpangokazi unaoaminiwa na wananchi wakati akilihutubia bunge waziri mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.