rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Watoto wengi kusini mwa DRC hujishughuliza na shughuli ya kuchimba madini

media
Mgodi wa shaba Kolwezi, Kusini Mashariki mwa DRC AFP/GWENN DUBOURTHOUMIEU

Kampeni ya kuwaondoa watoto katika shughuli ya uchimbaji madini katika migodi mbalimbali Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo inaandaliwa hivi karibuni katika jimbo la Lualaba na Katanga ya juu.


Maelefu ya watoto wanaripotiwa kutumiwa katika uchimbaji madini katika maendo hayo. Kazi wanaofanya ni ngumu ikilinganishwa na umri wao. Kuna baadhi ambao wamefariki, baada ya kufukiwa na udongo.

Katika mgodi unaopatikana katika eneo la Kolwezi, kusini mwa DRC, ambapo kampuni COMUS inaendesha shughuli zake, mashahidi wanasema watoto wengi wanatumiwa kuchimba madini.

Kwa upande wa mahirika yanayotetea haki za watoto wanalaani tabia hiyo ya watoto kutumiwa katika uchimbaji wa madaini katika migodi mbalimbali, Kusini Mashariki mwa DRC.

"Tunakuja kila asubuhi kutafuta madini. Tukifaanikiwa, tunauza. Unaweza kuisafisha kabla ya kuuza, " amesema mmoja wa watoto hao.

Baadhi ya wazazi wanasema wamekosa fedha kwa ada ya shule ya watoto zao.

Hata hivyo watoto hao wanasema wamefaulu pa kubwa katika shughuli hiyo, na kuweza kukidhi mahitaji yao muhimu.