Pata taarifa kuu
EBOLA-DRC-WHO

Katibu mkuu UN Guterres aahidi kushikamana na DRC

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres ameanza ziara ya siku tatu nchini DRC katika eneo la mashariki ambapo amelenga kuonesha mshikamano na taifa hilo linalokabiliwa na makundi ya uasi na mlipuko wa maradhi ya Ebola.

Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Antonio guterres mara baada ya kuwasili mjini Goma August 31 2019
Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa Antonio guterres mara baada ya kuwasili mjini Goma August 31 2019 Daniel Tschube Ngorombi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Alipokeleewa na Leila Zerrougui,mjumbe wake maalum katika nchi ya DRC ambapo wawili hao hawakusalimiana kwa kupeana mikono wakizingatia kanuni za kuepuka kusambaa virusi vya Ebola.

Β 

Ziara hii inakuja Wakati idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imevuka 2000,huku mgonjwa wa Ebola aliyebainika kwenye nchi jirani ya Uganda akifariki dunia.
Β 

Kulingana na ripoti ya shirika la Afya Duniani (WHO), hadi Agosti 28 nchini DRC, visa 3004 vya maambukizi ya virusi vya Ebola vilithibitishwa na watu 1998 walifariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.