rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Libya G7

Imechapishwa • Imehaririwa

G7 yakiri kuhusika katika uhasama Libya na kutoa wito wa mazungumzo

media
Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya. Abdullah DOMA / AFP

Mkutano wa kilele wa nchi zilizostawi kiuchumi duniani (G7) ambao unamalizika leo Biarritz, kusini magharibi mwa Ufaransa umezitaka pande zinazohasimiana nchini Libya kuketi kwenye meza ya mazungumzo.


Taarifa kuhusu mgogoro wa Libya inatarajiwa kutolewa hivi leo. Hata hivyo tayari baadhi ya mambo muhimu kuhusu taarifa hiyo yamefhamika.

Viongozi wa G7 wanabaini kuwa hali hiyo hairidhishi nchini Libya ambapo wababe wawili, Waziri Mkuu Fayez el-Sarraj na Marshal Khalifa Haftar, wanakinzana.

Wajumbe wawili kama wapatanishi wanasubiri kuwatenganisha, ikiwa ni pamoja na mmoja kutoka Umoja wa Mataifa na mwengine kutoka Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa kwa pamoja. Chanzo cha kutoka Afrika, ambacho kilihudhuria mkutano wa ushirikiano wa G7 na Afrika jana, kimebaini kwamba kuna hali ya sintofahamu kwa upande wa Jumuiya ya kimataifa kuhusu suala la Libya.

Kuhusika katika mgogoro

Wanachama wa G7 wanakiri kuwa wanahusika katika mzozo wa sasa nchini Libya. Wanachama hao ndio waliingilia kati nchini Libya, chini ya agizo la Umoja wa Mataifa, mnamo mwaka 2011. Na wanakubali kwamba kupinduliwa kwa Muammar Gaddafi kulisababisha ukosefu wa usalama katika Ukanda mzima wa Sahel.

Katika taarifa hiyo, G7 inatarajia kutoa wito kulingana na duru a kuaminika, wa kufanyika mkutano wa kimataifa kuhusu Libya ili kuleta pamoja nchi zote zinazohusika kwa njia moja ama nyingine katika mgogoro wa Libya, kama nchi za Ghuba.