rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

Imechapishwa • Imehaririwa

Mkosoaji wa Mnangagwa atekwa nyara na baadae kuachiliwa

media
Polisi wakipiga doria katika mji wa Harare, Januari 20. REUTERS/Philimon Bulawayo

Mchekeshaji wa mitandaoni nchini Zimbabwe Samantha Kureya, maarufu kwa jina la 'Gonyeti' ametekwa na watu wasiojuliakana akiwa nyumbani kwake jijini Harare.


Ripoti zinasema kuwa baada ya kutekwa alipigwa na kujeruhiwa vibaya.

Kureya ambaye pia ni mwanahabari ameelezea namna wanaume watatu waliokuwa wamefunika nyuso zao walivyovamia nyumba yake na kumchukua kwenda kumtesa.

Amekuwa mkosoaji wa serikali ya Emmerson Mnanangwanga na jeshi la polisi kupitia vichekesho vyake.