Pata taarifa kuu
CAMEROON-HAKI-SIASA

Mwanaharakati Julius Sisiku Ayuk Tabe ahukumiwa kifungo cha maisha Cameroon

Mahakama ya kijeshi nchini Cameroon imemuhukumu kifungo cha maisha jela, kiongozi wa vuguvugu la eneo linalozungumza kingereza, Julius Sisiku Ayuk Tabe, hukumu ambayo wadadisi wa mambo wanasema huenda ikachochea machafuko zaidi.

Kiongozi wa vuguvugu la eneo linalozungumza Kiingereza Kamusi Julius Sisiku Ayuk Tabe.
Kiongozi wa vuguvugu la eneo linalozungumza Kiingereza Kamusi Julius Sisiku Ayuk Tabe. YouTube
Matangazo ya kibiashara

Tabe anayeonekana kama kiongozi mwenye msimamo wa kati katika vuguvugu linalodai eneo hilo kujitenga, amehukumiwa sambamba na watu wengine 9 kwa makosa ya ugaidi na kuendesha harakati hatari kwa usalama wa taifa.

Hukumu hii imethibitishwa na wakili wa vuguvugu hilo, Joseph Fru, ambaye amesema watu wengine 10 walitakiwa kulipa faini ya CFA bilioni 250, sawa na dola za Marekani milioni 422.

Fru hata hivyo amelaani kile alichosema hukumu ya kushangaza na kwamba wateja wake wote wamekataa kutambua mamlaka ya mahakama ya kijeshi iliyokuwa inasikiliza kesi hiyo mjini Yaounde.

Tabe mwenye umri wa miaka 54 na mtaalamu wa masuala ya TEHAMA, alijitangaza kama rais wa Ambazonia, jimbo lililojitenga na Cameroon mwezi October 2017, ambapo Serikali iliingilia kati kwa kutuma wanajeshi ambapo watu elfu 1 na 800 waliuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.