rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • China ni yao pekee ambayo inaweza kutoa suluhu kwa katiba ya Hong Kong (Msemaji wa Bunge)

DRC Felix Tshisekedi

Imechapishwa • Imehaririwa

Tshisekedi aombwa kutimiza ahadi yake ya kurejesha usalama mashariki mwa DRC

media
Vijana, wenye hasira, wakiandamana mbele ya ikulu ya rais, mjini Kinshasa, Agosti 19, 2019, kutokana na kudorora kwa usalama mashariki mwa DRC. Pascal Mulegwa /RFI

Mamia ya vijana waliokasirishwa na hali mbaya ya usalama mashariki mwa DRC, wameandamana hapo jana Jumatatu, mbele ya ofisi ya rais Felix Tshisekedi Tshilombo mjini Kinshasa, kumshinkiza atimize ahadi yake ya kampeni ya kuimairisha usalama mashariki mwa nchi hiyo.


Wakizungumza na RFI jijini Kinshasa baadhi ya vijana wamesema kuwa wameandamana kwa lengo la kumkumbusha Rais Felix Tshisekedi ahadi yake wakati wa kampeni kwamba atahakikisha usalama unarejeshwa katika wilaya ya Beni, katika Mkoa wa Kivu kaskazini, lakini pia katika Mkoa wa Kivu Kusini na Ituri, mikoa ambayo imekabiliwa na mauaji ya mara kwa mara, na mapigano yasiyokoma kwa zaidi ya miaka ishirini sasa.

Mbunge Tembos Yotama amesema maelfu ya watu wamepoteza maisha, Huku maelfu ya wengine wamelazamika kuyatoroka makaazi na mali zao kutokana na kudorora kwa usalama, hata kwa waliosalia, wanaishi wakihofia usalama na maisha yao.

Katika mkutano wa SADC uliohitimishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Rais Felix Tshisekedi alipendekeza kuundwa kwa kikosi cha kikanda kitakachosaidia katika kushughulikia usalama kwenye mataifa wanachama, huku akisema anajaribu kutathmini ni vipi anaweza kuleta amani kwa taifa hilo, hasa zaidi katika eneo la Mashariki ambako kumeshuhudiwa ghasia na umwagikaji damu mkubwa wa raia, na uwepo wa wanamgambo waliojihami wanaotekeleza mashambulio.