Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-USALAMA

Burkina: Askari wengi wauawa katika "shambulio

"Makundi ya magaidi" yaliojihami kwa bunduki yameshambulia vikosi vya jeshi la Burkina Faso na kuua baadhi ya askari na wengine wengi kujeruhiwa, kwa mujibu wa byanzo kadhaa vya usalama nchini humo.

Mkoa wa Soum, kaskazini mwa Burkina Faso, ambapo shambulio hilo lilitokea Jumatatu Agosti 19.
Mkoa wa Soum, kaskazini mwa Burkina Faso, ambapo shambulio hilo lilitokea Jumatatu Agosti 19. © Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea mapema Jumatatu asubuhi, Kaskazini mwa nchi.

Uongozi wa jeshi la Burkina Faso umeandika kwenye taarifa kwamba kambi ya jeshi ya Koutougou katika Mkoa wa Soum imelengwa kwa "shambulio kubwa" na "makundi ya kigaidi yaliyojihami kwa bunduki".

Watu waliojihami kwa bunduki ambao walikuwa kwenye pikipiki na magari walifika kwenye eneo la mpakani na Mali, kulingana na chanzo cha usalama.

Shambulio hili, kwa uhakika, limeua askari wasiozidi kumi na mbili kulingana na taarifa iliyotolewa na uongozi wa jeshi. Lakini vyanzo kadhaa vya usalama vinaeleza kwamba askari ishirini ndio waliuawa katika shambulio hilo. Wanajeshi kadhaa pia wamejeruhiwa na wengine wengi wamekosekana. Vifaa vya jeshi vilichomwa moto na silaha kadhaa zilibebwa na washambuliaji.

Kwa mujibu wa uongozi wa vikosi vya jeshi vya Burkina Faso, operesheni kubwa ya jeshi iliendeshwa kujibu shambulio hilo. Washambuliaji wengi waliouawa na wengine wengi kukamatwa, taarifa ya jeshi imeeleza.

Kwa kuelezea mshikamano wake na vikosi vya ulinzi na usalama, serikali ya Burkina Faso, kupitia msemaji wake, imethibitisha azimio lake la kuhakikisha usalama wa watu na mali unapatikana kote nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.