rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Libya Uturuki Fayez al Sarraj Khalifa Haftar Recep Tayyip Erdogan

Imechapishwa • Imehaririwa

Libya: Ndege za majeshi ya Haftar zashambulia uwanja wa ndege wa Zouara

media
Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita Mashariki mwa Libya. © Abdullah DOMA / AFP

Mapigano nchini Libya yameanza tena baada ya siku chache kukubaliana kusitisha mapigano kwa muda kutokana na sikukuu ya Eid al-Kebir. Wakaazi wa baadhi ya maeneo wameanza kuyakimbia makaazi yao kufuatia mapigano hayo.


Alhamisi, Agosti 15, ndege za majeshi ya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita mashariki mwa Libya ziliendesha mashambulizi ya anga dhidi ya uwanja wa ndege wa Zouara.

Kwa mujibu wa majeshi ya Haftar, ANL, ndege zisizo kuwa na rubani za Uturuki zimekuwa zikiendesha mashambulizi ya angani dhidi ya majeshi yake yanayopiga kambi Kusini mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli, zikitokea kwenye uwanja huo wa ndege wa Zouara.

Uturuki inahusika sana katika vita vinavyoendelea nchini Libya.

Uturuki inaendesha operesheni zake hadharani nchini LIbya. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekiri mara kadhaa kuunga mkono Fayez al-Sarraj, Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Marshal Khalifa Haftar alilaani mara kadhaa uingiliaji kati huo wa Uturuki nchini Libya, ambao ulisababisha mzozo kati ya Ankara na Benghazi mapema mwezi Julai mwaka huu.

Ankara haikutuma tu magari kadhaa ya kijeshi, lakini pia makombora na ndege zisizokuwa na rubani aina ya Bayraktar kwa wanamgambo wanaounga mkono serikali ya umoja wa kitaifa ya Tripoli.