Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Serikali nchini DRC: Raia waendelea kuwa na uvumilivu

Wananchi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea kusubiri kutangazwa serikali mpya, serikali ya kwanza katika utawala wa Felix-Antoine Tshisekedi Tshilombo.

Wakaazi wengi wa mji wa Kinshasa waendelea kusubiri kuundwa kwa serikali ya kwanza katika utawala wa Felix Tshisekedi (kwenye picha).
Wakaazi wengi wa mji wa Kinshasa waendelea kusubiri kuundwa kwa serikali ya kwanza katika utawala wa Felix Tshisekedi (kwenye picha). © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu wengi wanalalamika kuhusu kucheleweshwa kwa serikali hiyo na hivyo kusababisha hali ya sintofahamu nchini humo.

Wengi wameanza kukata tamaa, huku wengine wakionekana ni wenye hasira, na wengine kuwa na wasiwasi kwa kusubiri kutangazwa kwa baraza jipya la mawaziri.

Wachambuzi, wachanganuzi, wadau mbalimbali wote wamekuwa na wasiwasi kufuatia hali hiyo ya kuchelewa kutangazwa serikali nchini DRC, anasema José Nawej kutoka shirika la kiraia la Forum des As.

Kwa upande wa raia, wengi wamekata tamaa. Tumechoka na kusubiri serikali mpya, baada ya zaidi ya miezi saba, tukisalia bila serikali, shughuli nyingi za serikali zikisimamiwa na serikali ya utawala wa zamani wa Joseph Kabila, wakazi wengi wa mji wa Kinshasa wamesem , huku wakisema kushangazwa na hali hiyo.

Matokeo: Daktari, jaji au mfanyabiashara, kila mtu anasubiri serikali kwa matumaini ya kurekebisha hali hiyo katika sekta zote. Kwa upande wa wafanyakazi wa serikali, wanasema wana matumaini kuwa mishahara itaongezwa kwa kiwango cha kuridhisha. Rais Félix-Antoine Tshisekedi aliahidi kuongeza mishahara wakati wa kampeni za uchaguzi, François, afisa katika Wizara ya Utalii, anakumbusha.

Wanajeshi na polisi, wale ambao wako chini ya bendera, wanaendelea kusubiri zaidi. Wakati wa matangazo ya runinga, mke wa mwanajeshi mmoja alitokwa na machozi, akiomba watoto wa wale wanaojitolea maisha yao kwa kudumisha usalama nchini waweze kusaidiwa kuhudumiwa katika masuala ya shule, hususan karo ya shule na membo mengine. Tangu wakati huo, picha ya mwananke huyo inaendelea kurushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Ikiwa zimesalia wiki mbili tu kabla ya kuanza kwa mwaka wa shule, suala hili la elimu ya bure kwa watoto linaongoza katika mijadala mbalimbali nchini DRC. Kinachobaki ni kusubiri kujua majina ya mawaziri wa serikali ijayo ambao watateuliwa kwenye nafasi hizo zenye maswala haya mengi yanayopewa kipaumbele.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.