Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Wananchi wa DRC waendelea kusubiri serikali mpya

Mpaka sas hakuna taarifa yoyote kuhusu kuundwa kwa serikali mpya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga anatarajia kuwasilisha kwa rais Felix Tshisekedi Tshilombo majina ya watu waliopendekezwa kuhudumu kwenye nafasi za mawaziri kwenye srikali hiyo mpya.

Rais Felix Tshisekedi (kulia) Na Waziri Mkuu mpya Sylvester Ilunga Ilunkamba.
Rais Felix Tshisekedi (kulia) Na Waziri Mkuu mpya Sylvester Ilunga Ilunkamba. @ Présidence de la République démocratique du Congo
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi wa mawaziri unatarajiwa wiki hii. Viongozi wa makundi 21 na chama cha siasa vinavyojumuika kwenye muungano FCC wamekutana na Seneta wa milele Joseph Kabila, ambaye ni nguzo ya muungano huo kwa kuzungumza kuhusu mgawanyo wa majukumu katika serikali mpya ijayo.

Kulingana na vyanzo vya karibu na muungano wa FCC, nafasi za mawaziri zilitolewa kulingana na idadi ya wabunge ambao kila chama kinao katika Bunge la Kitaifa.

Pamoja na wabunge 118 katika ngazi ya taifa, chama cha PPRD kitachukuwa nafasi za mawaziri 11 na manaibu mawaziri 3. muungano wa AAB unaojumuisha vyama kadhaa vya siasa katika muungano wa FCC, utaweza kupata mawaziri watatu na naibu waziri, vyama vingine vinaweza kuwa na waziri mmoja au wawili au naibu waziri, kulingana na chanzo hicho.

Makundi matatu ambayo hayana wawakilishi bungeni hayataweza kuwakilishwa katika serikali hiyo mpya.

Kwa upande mwingine, wafuasi wa chama cha AFDC ambao wameendelea kushirikiana na Joseph Kabila watnaweza kuwakilishwa serikalini. Joseph Kabila anapaswa kunufaika na kiwango cha 10% kwenye nafasi 42 zilizohifadhiwa kwa washirika wake wa kisiasa.

Hata hivyo, orodha ya majina ya watu watakaoshirikishwa katika serikali ijayo imezua mgawanyiko mkubwa katika muungano wa vyama vya kisiasa vya Palu na washirika wake. Naibu kiongozi wa kwanza wa muungano huo, Elvis Mutiri na maafisa wengine wawili, Henri Thomas Lokondo na Richelieu Lumumba, hawakubaliani na katibu mkuu wa Palu ambaye amewasilisha kwa muungano huo majina ya watu kutoka chama cha Antoine Gizenga kushirikishwa katika serikali mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.