Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGAIDI-USALAMA

Burkina: Serikali yataka kulinda mshikamano wa kijamii dhidi ya ugaidi

Burkina Faso inaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka 2015. Machafuko ya kijamii ambayo yamesababisha watu wengi kupoteza maisha, uharibifu mkubwa wa mali na watu kulazimika kuyatoroka makazi yao pia yanajiongeza kwa hali hiyo.

Maandamano mbele ya mahakama ya mjini Ouagadougou, waandamanaji wanaomba "ukweli na haki" baada ya shambulio la kigaidi Januari 1, 2019 kaskazini mwa Burkina Faso.
Maandamano mbele ya mahakama ya mjini Ouagadougou, waandamanaji wanaomba "ukweli na haki" baada ya shambulio la kigaidi Januari 1, 2019 kaskazini mwa Burkina Faso. OLYMPIA DE MAISMONT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mdororo huo wa usalama unatatiza mshikamano wa kijamii.

Kutokana na hali hiyo, serikali na wawakilishi wake wameanza kukutana kwa mazungumzo kutafutia ufumbuzi kuhusu mdororo huo wa usalama na kufikiria namna ya kuimarisha usalama.

Magavana na makamishna wakuu wameiambia serikali kwamba migogoro ya kijamii inazidi kutumiwa na magaidi. Na hali hii inatishia mshikamano wa kitaifa, kulingana na Antoine Atiou, msemaji wa magavana. "Kulikuwa na mazungumzo ya jinsi ya kupitisha mikakati ya ubunifu ya kudhibiti mzozo huu na migogoro mbalimbali, ikiwa inawezekana, kukomesha kabisa, " amesema Antoine Atiou.

Waziri Mkuu wa Burkina Faso, Christophe Dabiré, pia amehakikisha kwamba mkakati wa kitaifa wa kupambana dhidi ya itikadi kali unaendelea.

"Mpango wa utekelezaji, ikiwa uko tayari, utapitishwa, na tutatoa uwezo ili mshikamano wa kijamii uwe kwenye ajenda ya mazungumzo ambayo tutakuwa nayo na wadau wote kuhusu suala hili", amesema Waziri Mkuu.

Baada ya kmazungumzo ya moja kwa moja na Waziri Mkuu, magavana na makamishna wakuu wamepongeza hatua hii ya serikali katika mfumo wa kuzuia na kudhibiti machafuko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.