rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

DRC Joseph Kabila Felix Tshisekedi

Imechapishwa • Imehaririwa

DRC yasubiri uamuzi wa mwisho kwa kuundwa serikali mpya

media
Rais Felix Tshisekedi (kulia) Na Waziri Mkuu mpya Sylvester Ilunga Ilunkamba. Présidence de la République démocratique du Congo

Kwa wakati wowote kuanzia sasa serikali mpya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itatangazwa. Waziri Mkuu Sylvester Ilunga Ilunkamba anatarajia Jumanne wiki hii kukabidhi majina ya watu alioteuwa kushiriki katika serikali ijayo kwa rais Felix Tshisekedi, kabla ya uteuzi rasmi.


Orodha ya watu watakaoteuliwa kwenye nafasi ya mawaziri iko mikononi mwa Waziri Mkuu tangu Jumapili, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Orodha hiyo, iliyopendekezwa na miungano miwili ya vyama vya siasa, FCC , unaoongozwa na Joseph Kabila na CACH wa rais Tshisekedi, itapelekwa kwa Félix Tshisekedi kwa kuisahihisha.

Katika saa 48 zilizopita, Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga Ilunkamba aliteuwa majina hayo kwa vigezo vilivyokubaliwa na rais wa Jamhuri na mwenyekiti mwenye mamlaka wa FCC, Joseph Kabila.

Majina zaidi ya mia moja yataangaliwa na kupitiwa upya, lakini majina 65 pekee ndio yanatakiwa na rais, ambaye ana mamlaka ya kuteua serikali.

"FCC, tuna uhakika tumetoa majina ya watu, wanawake kwa wanaume wenye uwezo wa kufanya kazi. Joseph Kabila amepata wakati wa kupitisha orodha hii na kwa hiyo hakuna mazungumzo yoyote yanayotarajiwa," amesema afisa mwandamizi wa FCC, ambaye hakutaja jina lake.

Muungano wa CACH utapata nafasi 23, na FCC itapata nafasi 43.