Pata taarifa kuu
CHAD-USALAMA

Watu 37 wauawa katika mapigano ya kikabila Chad

Watu 37 wamepoteza maisha nchini Chad baada ya kuzuka kwa mapigano mapya ya kikabila, Mashariki mwa mkoa wa Ouaddie. Rais Idriss Deby ametangaza kutokea kwa mauaji hayo, baada ya kuzuka kwa mapigano ya siku tatu katika mkoa huo unaopakana na nchi jirani ya Sudan.

Polisi akipiga doria karibu na soko kuu la N'Djamena, kwenye eneo la shambulio Julai 11, 2015.
Polisi akipiga doria karibu na soko kuu la N'Djamena, kwenye eneo la shambulio Julai 11, 2015. REUTERS/Moumine Ngarmbassa
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na Wanahabari jijini Ndjamena, rais Derby amesema mapigano ya kikabila nchini, limekuwa sasa suala ambalo linatia wasiwasi .

Mapigano hayo yameshuhudiwa kati ya kabila la kuhamahama la Zaghawa linalofunga ngamia na wakulima kutoka kabila la Ouaddian .

Imekuwa ni wiki ya mapigano katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo, na hospitali moja imeripoti kuwa watu walipoteza maisha ni 44.

Polisi waliokwenda kutuliza ghasia, walishambuliwa kwa risasi, suala ambalo rais Deby amesema halikubaliki na amepanga kuzuru eneo hilo hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.