rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Tunisia Beji Caid Essebsi

Imechapishwa • Imehaririwa

Waziri wa Ulinzi wa Tunisia kuwania kiti cha urais

media
Mmoja wa wananchi wa Tunisia akisoma gazeti kuhusu kifo cha rais wa nchi hiyo Beji Caid Essebsi. REUTERS/Zoubeir Souissi

Waziri wa Ulinzi nchini Tunisia, Abdelkarim Zbidi, amewasilisha maombi ya kuwania urais, wakati uchaguzi utakapofanyika nchini humo tarehe 15 mwezi Septemba.


Waziri huyo amesema atajiuzulu kama Waziri na atawania wadhifa huo kama mgombea binafsi.

Zbidi, mwenye umri wa miaka 69, anaungwa mkono na vyama mbalimbali ikiwa ni pamoja na Nidaa Tounes na Afek Tounes, huku akitarajiwa kuwa miongoni mwa wagombea watakaoonyesha upinzani mkubwa uliotisha baada ya kufariki rais wa nchi hiyo Beji Caid Essebsi mwezi uliopita.

Zbidi, ni dakatari kitaaluma na anatajwa kuwa miongoni mwa watu waliochangia mageuzi ya kiuchumi kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.

Waziri huyo anatarajiwa kuonyesha upinzani mkubwa kwa Waziri Mkuu wa sasa Youssef Chahed ambaye atagombea urais kupitia chama cha Liberal Tahya Tounes Party.

Wagombea wengine katika uchaguzi huo ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Mehdi Jomaa na Moncef Marzouki, ambaye alihudumu kama rais wa muda katika kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2011.