rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Congo Brazzaville

Imechapishwa • Imehaririwa

Mtoto wa Sassou-Nguesso ashtumiwa ubadhirifu wa dola milioni 50

media
Mtoto wa Rais wa Congo Denis Sassou-Nguesso anatuhumiwa na shitika lisilo la kiserikali la Global Witness kupitisha mlango wa nyuma Dola milioni 50 katika mali ya umma. © AFP/AFP

Shirika lisilo la kiserikali la Global Witness linamshutumu, katika ripoti iliyofichuliwa Jumanne wiki hii, Agosti 6, mtoto wa Rais wa Congo Denis Christel Sassou-Nguesso, kupitisha mlango wa nyuma karibu dola milioni 50 katika mali ya umma.


Kwa mujibu wa Global Witness, kati ya mwaka 2013 na 2014, Denis Christel Sassou-Nguesso alipitisha mlango wa nyuma Dola milioni 50 katika mali ya umma kupitia makampuni yenye makao yao nchini Cyprus.

Kwa mujibu wa Global Witness, Gabox, moja ya makampuni hayo yalinufaika kutokana na mkataba wa uwongo ili kushiriki katika kuchapisha ramani ya jiografia ya Jamhuri ya Congo na kampuni hiyo, ambayo ni mali ya Denis Christel Sassou -Nguesso.

"Serikali ya Congo ilisaini mkataba na kampuni ya Asperbras kutoka Brazil na kisha Asperbras ikasaini mkataba wa uwongo na kampuni ya Denis Christel Sassou-Nguesso yenye makao yake nchini Cyprus inayoitwa Gabox. Hii ni kampuni hewa ambapo jina la Denis Christel lilifichwa, "amesema Mariana Abreu ambaye anahusika na kampeni katika shirika la Global Witness.