rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Libya Mauaji

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 40 wauawa katika shambulio la anga Libya

media
Libya yaendelea kukumbwa na mapigano kati ya jeshi la serikali ya umoja na wapiganaji wa Marshal Khalifa Haftar. AFP / LNA WAR INFORMATION DIVISION

Watu 40 wameripotiwa kupoteza maisha nchini Libya na wengine kujeruhiwa baada ya kushambuliwa wakiwa wanahuhudria sherehe ya harusi Kuisni Magharibi mwa nchi hiyo.


Ripoti zinaeleza kuwa waliotekeleza mashambulizi hayo ya angani ni wapiganaji wa kiongozi wa upinzani Khalifa Haftar anayeendeleza harakati za kutaka kudhibiti jiji kuu Tripoli na kuchukua uongozi w ataifa hilo.

Ni mwendelezo wa mauaji ambayo yanaendelea kutelezwa na vikosi vya Haftar tangu mwezi Aprili, ambapo hadi sasa takwimu zinaoeneha kuwa zaidi ya watu elfu moja wamepoteza maisha.

Jumuiya ya Kimataifa imeendelea kusaidia kuleta pamoja, pande hizi mbili zinazozana bila mafanikio huku, serikali inayotamvuliwa Kimataifa ikitangaza ushindi dhidi ya vikosi vya Fajtari mara kwa mara.

Tangu kuuawa na kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muakar Kdhafi mwaka 2001, Libya haijawa tulivu.