rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani

Imechapishwa • Imehaririwa

Mkataba kuhusu taasisi za mpito kutiliwa saini Agosti 17 Sudan

media
Wananchi wa Sudan washerehekea hatua ya utiliaji saini kati ya uatawala wa kijeshi na viongozi wa maandamano. Ebrahim HAMID / AFP

Wananchi wa Sudan wamekuwa wakisherehekea hatua iliyofikiwa kati ya utawala wa kijeshi na viongozi wa maandamanoJumapili wiki hii kuelekea utiwaji saini rasmi tarehe 17 mwezi huu, siku ambayo rais wa zamani Omar Al Bashir anatarajiwa kupelekwa Mahakamani.


Inatarajiwa kuwa baada ya tarehe 17 wanajeshi na viongozi wa serikali wataunda serikali hiyo ya mpito.

Wanajeshi na viongozi wa waandamanaji nchini Sudan, hatimaye wametiliana saini mkataba wa kikatiba utakaowaongoza katika serikali ya mpito, baada ya miezi saba ya mzozo wa kisiasa.

Mkataba huo unaweka wazi namna taifa hilo litakavyoelekea katika serikali ya kiraia, baada ya serikali ya mpito kumalizika baada ya miaka mitatu.

Kiongozi wa waandamanaji Ahmed Rabie na naibu kiongozi wa Baraza la Kijeshi Jenerali Mohamed Hamdan Daglo, ndio waliotia saini mkataba huo ulioshuhudiwa na wasuluhishi kutoka nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika.