Pata taarifa kuu
SUDAN-BASHIR-RUSHWA-HAKI

Sudani: Kesi ya rushwa inayomkabili Omar al-Bashir kufunguliwa Agosti 17

Kesi ya rushwa inayomkabili aliyekuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir, aliyetimuliwa mamlakani mwaka huu itafunguliwa Agosti 17. Omar al-Bashir anayeshtakiwa kwa ufisadi hakuwasili mahakamani leo Jumatano, kesi ambayo ingesikilizwa kwa mara ya kwanza, amesema mmoja wa mawakili wake.

Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa mahojiano na televisheni ya taifa Februari 3, 2012.
Aliye kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa mahojiano na televisheni ya taifa Februari 3, 2012. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

"Leo ilikuwa kesi ya mteja wetu ingesikilizwa kwa kwanza, lakini viongozi hawakuweza kumleta kwa sababu za kiusalama, kwa hivyo jaji ametuarifu kwamba kesi hiyo itasikiloizwa Agosti 17 ", Wakili Hicham al-Gaaly ameliambia shirika la Habari al AFP.

Kwa upande wa Ahmed Ibrahim al-Tahir, wakili wake mwengine, amesma kesi hiyo haina "sio ya kisiasa"."Ni kesi ya jinai na tuhuma zinazomkabili hazina msingi," amesema.

Mnamo Juni 16, mwendesha mashtaka alisoma mashtaka dhidi ya rais huyo wa zamani, wakati aliponekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu kutimuliwa mamlakani na jeshi Aprili 11.

Tangu wakati huo Bashir anashikiliwa mahabusu na anashtumiwa "kumiliki katika njia haramu fedha za kigeni", "kupata utajiri kwa njia haramu", kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka.

Kwa mujibu wa Tahir, moja ya mashtaka yanahusu jumla ya Euro milioni saba zilizotolewa "na wafadhili, ambazo hazikujumuishwa kwenye bajeti ya serikali."

Mwishoni mwa mwezi Aprili, mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, alidai kwamba Dola sawa na zaidi ya milioni 113 taslimu zilikamatwa katika makazi ya Omar al-Bashir jijini Khartoum.

Alisema polisi, jeshi na maafisa wa usalama walipata Euro milioni saba, dola milioni 350,000 na Pauni za Sudani milioni tano (sawa na Euro milioni 93) wakati wa msako huo.

Bw Bashir aliingia madarakati kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 1989, alitimuliwa na kukamatwa na jeshi Aprili 11 jijini Khartoum, chini ya shinikizo la maandamano ya kipekee yaliyozuka mwezi Desemba kufuatia kuongezwa mara dufu kwa bei ya mkate.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.