Pata taarifa kuu
DRC-WHO-EBOLA-AFYA

WHO yatangaza Ebola kuwa ni janga la kimataifa

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza "dharura ya kiafya" duniani kwa sababu ya ugonjwa wa Ebola nchini DRC ambao umeua watu 1,668 tangu mwezi Agosti mwaka jana.

Afisa wa afya DRC akitoa chanjo ya ugonjwa wa Ebola katika kituo cha afya cha Himbi, Goma, DRC, Julai 17, 2019.
Afisa wa afya DRC akitoa chanjo ya ugonjwa wa Ebola katika kituo cha afya cha Himbi, Goma, DRC, Julai 17, 2019. © REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Tahadhari hii imetolewa baada ya mtu wa kwanza kufariki dunia  baada ya kubainika kuwa aliambukizwa virusi vya Ebola katika mji wa Goma, mji unaotembelewa na watu kutoka nchi mbalimbali kutoka za Maziwa Makuu.

Uamuzi wa kutangaza dharura kiafya duniani umechukuliwa na jopo la wataalamu wa shirika la Afya Duniani, WHO. Shirika la Afya Duniani limezingatia vigezo kadhaa, ambavyo kwanza ni hatari ya kusambaa kwa virusi vya Ebola duniani.

Katika kesi ya ugonjwa wa Ebola, tamko hili la dharura ya kiafya duniani linaonyesha wasiwasi wa wataalam kuona ugonjwa huo unasambaa katika nchi nyingine.

Mgonjwa aliyeambukizwa virusi vya Ebola alifariki dunia siku ya Jumatatu wakati alipokuwa akisafirishwa kutoka Goma kwenda Butembo, katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC. Jiji la Goma, ambalo lina wakaazi milioni 1, liko kwenye mpaka na Rwanda. Uwanja wake wa ndege pia unapokea abiria kwenda na kutoka Kinshasa au Addis Ababa.

Shirika la Afya Duniani linasema virusi vya ugonjwa huo vinaendelea kusambaa kutoka Afrika Magharibi na sasa kufikia nchi nyingine. Mataifa mengi yameimarisha ukaguzi katika viwanja vya ndege.

Lakini shirika hilo limesema hatari ya ugonjwa huo kusambaa nje ya Congo si kubwa.

Wakati huo huo raia wa miji miwili ya Goma mashariki mwa Congo na Gisenyi nchini Rwanda wamezitaka serikali za mataifa hayo mawili kuongeza vifaa vya uchunguzi wa homa ya Ebola kwenye mipaka.

Mlipuko wa Ebola ni ugonjwa wa pili kwa ukubwa katika historia ya nchi hiyo, ulianza mwezi Agosti na inaathiri mikoa miwili nchini DRC, Kivu Kaskazini na Ituri.

Zaidi ya watu 2500 wameathiriwa na ugonjwa huo na theluthi mbili kati yao wamepoteza maisha.

Ilichukua siku 224 kwa idadi ya walioathirika kufika 1,000 , lakini ndani ya siku 71 zaidi idadi ilifika 2,000.

Watu takribani 12 huripotiwa kupata ugonjwa huo kila siku.

Wafanyakazi wa afya wamekua wakipata vikwazo vya kutoaminika na machafuko nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.