Pata taarifa kuu
SUDANI-MAZUNGUMZO-SIASA-USALAMA

Sudan: Mazungumzo yaanza tena kati ya jeshi na upinzani

Mazungumzo kati ya jeshi linaloshikilia madaraka na viongozi wa maandamano yameanza tena Jumatano wikii hii katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Wawakilishi wa Baraza la Jeshi la Sudan na waandamanaji wamekutana katika Hoteli ya Corinthia, Khartoum tarehe 3 Julai 2019.
Wawakilishi wa Baraza la Jeshi la Sudan na waandamanaji wamekutana katika Hoteli ya Corinthia, Khartoum tarehe 3 Julai 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya ni ya kwanza kati ya pande hizo mbili tangu jeshi kusambaratisha waandamanaji waliokuwa wanapiga kambi kwenye makao makuu ya wizara ya ulinzi mapema Juni. Hatua hiyo ya jeshi ilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha.

Hata hivyo upande wa tume ya mseto ya usuluhishi inayoongozwa na Umoja wa Afrika na Ethiopia, wamesema hatua hiyo ya kuanza tenakwa mazungumzo ni ushindi, licha ya kuwa bado kuna kazi kubwa ya kuzikinaisha pande husika kukubali kuunda serikali ya mpito.

Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Corinthia, moja ya hoteli za mji mkuu, pembezoni mwa Mto Nile. Kwa mujibu wa shirika la Habari la AFP, Majenerali watatu wa Baraza la Kijeshi na wawakilishi 5 kutoka upande wa waandamanaji wameshiriki mazungumzo hayo.

Mapema Jumatano mchana, katika mkutano na waandishi wa habari, upinzani ulisema uko tayari kushiriki mazungumzo hayo kwa sharti kuwa makubaliano yafikiwe ndani ya saa 72.

Kusitishwa kwa mazungumzo kulisababishwa kwa kiasi kikubwa na muundo wa Baraza la uongozi wa nchi, ambapo kila upande unataka kuongoza.

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu ya mazungumzo hayo, baraza hilo litaundwa na askari 7, raia 7 na mtu mmoja ambaye atachaguliwa na pande hizo mbili. Kwa mujibu wa hati inayojadiliwa, jeshi litaongoza baraza hilo la uongozi wa nchi kwa kipindi cha miezi 18, kabla ya kukabidhi madaraka kwa raia. Kwa Jumla uongozi wa mpito utadumu miaka mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.