rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
Haraka
Vituo vya kupigia kura vyafunguliwa nchini Israeli: Wapiga kura milioni 6 wanapiga kura katika Uchaguzi Mkuu kuwachaguwa wabunge

Libya UNSC

Imechapishwa • Imehaririwa

Shambulio dhidi ya wahamiaji Libya: UNSC yashindwa kuafikiana

media
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano maalum Septemba 26, 2018 New York. REUTERS/Eduardo Munoz

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kutoa tamko kuhusu shambulizi la anga lililotekelezwa na wapiganaji wa Marshal Khalifa Haftar ambapo wahamiaji haramu zaidi ya 40 wameuawa katika shambulio la anga dhidi ya kambi yao katika moja ya vitongoji vya mji wa Tripoli.


Watu 70 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Haya yanajiri wakati mkuu wa kamati ya Baraza la Seneti la Marekani ametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu silaha za nchi hiyo zilizotumiwa na jeshi la jenerali muasi wa Libya Khalifa Haftar.

Jumanne wiki hii Umoja wa Mataifa ulisema kuwa mashambulizi ya Jumatatu nchini Libya, ambayo yamewaua takribani watu 40 katika mji wa Tripoli, yanaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita.

Kwenye taarifa yake, Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Ghassan Salame, amesema ni dhahiri kuwa mashambulizi hayo yanaweza kuwa uhalifu wa kivita kwa sababu yaliuwa kwa ghafla, watu ambao hawakuwa na hatia, na ambao hali yao mbaya ndiyo iliwalazimu kuwa katika kituo hicho cha wakimbizi.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, ametaka uchunguzi huru ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliohusika na uhalifu huo wa kusikitisha.