rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Syria: Raia 14 wauawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki na washirika wake (ripoti mpya ya OSDH)
  • Afghanistan: Karibu watu 62 wauawa katika shambulio dhidi ya msikiti, mashariki mwa nchi (mamlaka)

DRC WHO Ebola Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

Shirika la Afya Duniani WHO lafunga milango Beni

media
Maafisa wa afya wa DRC na wale wa Shirika la Afya Duniani wakivalia mavazi ya kujikinga dhidi ya Ebola wakati walipokuwa wakishiriki katika mafunzo ya kupambana dhidi ya Ebola karibu na mji wa Beni Agosti 11, 2018. REUTERS/Samuel Mambo

Shirika la afya duniani WHO, limetangaza kusitisha shughuli zote za kutoa huduma za afya katika eneo la Beni, lililoathiriwa na ugojwa hatari wa Ebola.


Mkuu wa operesheni za dharura za WHO barani Afrika na katika eneo la Ituru na Kivu Kaskazini, Daktari Michel Yao, ametangaza hatua hiyo baada ya vijana wenye hasira kuteketeza moto gari lao katika Manispaa ya Mulekera.

Hali hiyo imeleta wasiwasi mkubwa katika maeneo ya Beni, huku maafisa wa faya wakuhofia usalama wao.

Aidha, Daktari huyo amesema kuwa katika mazingira hayo, ni vigumu kuendelea kufanya kazi kwa sababu wahudumu wa afya wanahofia maisha yao.

Hatua hii inakuja, baada ya ripoti kuwa watu 1,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo tangu mwezi Agosti mwaka uliopita, Mashariki mwa nchi hiyo.

Watu wengine zaidi ya elfu mbili, wameambukizwa na laki moja na elfu aroboini kupewa chanjo.