rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Karibu kesi 6,000 ya udhalilishaji wa kingono ziliripotiwa Uber nchini Marekani mwaka 2017 na 2018 (rasmi)

Misri Uturuki Mohamed Morsi

Imechapishwa • Imehaririwa

Misri yagadhabishwa na kauli ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

media
Waziri wa Mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry wikipedia

Waziri wa Mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry amelaani kauli ya rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi alihusika na kifo cha rais wa zamani Mohamed Morsi.


Shoukry amesema kauli ya Erdogan haikubali na imetolewa kwa nia mbaya.

“Morsi alikuwa mwenye maumivu, akiwa kwenye sakafu kwa dakika 20 na kwa bahati mbaya, hakuna kilichofanyika kumsaidia,” alisema Erdogan.

“Morsi aliuawa. Hakuna kwa sababu za kiasili.”

Morsi alifariki dunia baada ya kuzirai akiwa Mahakamani siku ya Jumatatu, na kuzikwa jijini Cairo siku ya Jumanne, mazishi yaliyohudhuriwa na familia yake peke yake.

Erdogan alikuwa mshirika wa karibu wa Morsi kwa kipindi cha mwaka mmoja alipokuwa madarakani kabla ya kuondolewa madarakani mwaka 2013.

Tangu kipindi hicho, uhusiano wa kidiplomasia kati ya Cairo na Ankara umeyumba.