Pata taarifa kuu
OLOMIDE-MUZIKI-TAMASHA-AFRIKA KUSINI

Matamasha ya Kofi Olomide nchini Afrika Kusini yafutwa

Matamasha mawili ya mwanamuziki Nguli wa miondoko ya Rumba nchini DRC Kofi Olomide yamefutwa huko nchini Afrika Kusini kutokana na kukutwa na makosa ya ubakaji hivi karibuni dhidi ya mnenguaji wake.

Koffi Olomidé
Koffi Olomidé Seyllou / AFP
Matangazo ya kibiashara

Olomide mwenye umri wa miaka 62 ambae jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba alitarajiwa kuwa na tamasha katika ukumbi wa Gallagher Convention Centre nje kidogo ya jiji la Johannesburg June 28 pamoja na lingine katika ukumbi wa the Shimmy Beach Club huko Cape Town siku mbili baadaye.

Baada ya kampeni ilioendeshwa kwenye mitandao ya kijamii, hatimae mkurugenzi wa ukumbi wa Gallagher Convention Center, Charles Wilson amesema katika taarifa yake kwamba tamasha la Koffi Olomide limefutwa.

Wakati huo, huo ukumbi wa Shimmy Beach nao umetangaza mapema kwamba tamasha la Koffi Olomide limefutwa.

Mwezi Machi mahakama ya jijini paris ilimuhukumu Olomide kifungo cha miaka 2 baada ya kesi ambayo hata hivyo hakuhudhuria.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimfutua tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanenguaji wengine 3 nyumbani kwake jijini Paris mwaka 2002-2006.

Olomide aliwahi kutiwa mbaroni kwa muda mfupi mwaka 2016 baada ya kumpinga mnenguaji wake jijini Nairobi nchini Kenya ambapo alihukumiwa kifungo cha mieizi mitatu jela mwaka 2012 baada ya kumpiga mtengenezaji wa muziki wake.

Polisi nchini Zambia inamtafuta Koffi Olomide kwa kosa la kumpiga mpiga picha rais wa Rwanda jijini Lusaka nchini Zambia mwaka 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.