rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • China ni yao pekee ambayo inaweza kutoa suluhu kwa katiba ya Hong Kong (Msemaji wa Bunge)

Mali Siasa Ibrahim Boubacar Keita

Imechapishwa • Imehaririwa

Mali yaimarisha usalama katika vijiji vilivyoshambuliwa na watu wenye silaha

media
Kijiji cha Sobane kilichoshambuliwa nchini Mali © REUTERS/Malick Konate

Jeshi nchini Mali, limeimarisha usalama katika vijiji vinavyokaliwa na kabila la Dogon, baada ya watu 41 kupoteza maisha baada ya kuvamiwa na watu wenye silaha.


Maafisa wa usalama wameonekana wakipiga doria katika eneo hilo baada ya mashambulizi hayo kushuhudiwa katika vijiji vya Gangafani na Yoro, siku ya Jumatatu wiki hii.

Mapigano yameendelea kushuhudiwa kati ya makabila ya Fulani na Dogon ambao ni wakulima na wafigaji.

Umoja wa Mataifa unasema mbali na watu waliopoteza maisha, kuna wengine 38 waliojeruhiwa.

Serikali ya Mali, imetuma wanajeshi wake kwenda kulinda raia katika vijiji hivyo na kuleta utulivu kwa sasa.

Tangu mwaka 2012, Mali imeendelea kushuhudia changamoto za kiusalama na Umoja wa Mataifa imetuma jeshi lake maarufu kama MINUSMA kwenda kupambana na makundi ya kigaidi.