Pata taarifa kuu
MISR-MORSI-UN-UNHRC

Misri yaushtumu Umoja wa Mataifa kuhusu kifo cha Morsi

Misri inaishtumu Umoja wa Mataifa kwa kutia siasa katika kifo cha rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini humo Mohamed Mors,i aliyezirai na kupoteza maisha akiwa Mahakamani jijiini Cairo siku ya Jumatatu.

Mohammed Morsi akiwa Mahakamani wakati wa uhai wake
Mohammed Morsi akiwa Mahakamani wakati wa uhai wake DR
Matangazo ya kibiashara

Cairo imetoa kaul hii baada ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za binadamu kutaka uchunguzi kufanyika kubaini kilichochangia kifo cha Morsi.

Wizara ya Mambo ya nje nchini Misri kupitia msemaji wake Ahmed Hafez, amelaani wito huo wa Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa, na kusema, haukubaliki.

Aidha, ameongeza kuwa Tume hiyo kwa makusudi imeamua kutia siasa kuhusu kifo cha Morsi ambacho kiliwashangaza wengi.

Msemaji wa Tume hiyo ya Haki za Binadamu Rupert Colville, ametaka ukweli kuwekwa wazi kuhusu hali ambayo Morsi alizuiwa kwa karibu miaka sita.

Kumekuwa na wasiwasi kuwa mazingira mabaya ya kibinadamu, kunyimwa haki ya kupata dawa na kutengwa kwa saa nyingi lakini pia kutoruhusiwa kuonana na familia yake, kulichangia pakubwa kifo chake.

'Kifo kinachotokea kizuizini, ni lazima kifuatiwe na uchunguzi wa kina ambao utakuwa wazi na huru ili kufahamu ukweli wa kilichotokea,” amesema Colville.

Mashirika ya kutetea haki za Binadamu yakiongozwa na Human Rights Watch yanailamu serikali ya Misri kwa kifo hicho kwa kile yachosema , Morsi alizuiwa katika mazingira magumu.

Alizikwa siku ya Jumanne jijini Cairo, baada ya serikali kukataa ombi la familia yake kwenda kumzika alikozaliwa.

Morsi aliondolewa madarakani na Mkuu wa Majeshi mwaka 2013, ambaye sasa ni rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.