Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-UGAIDI

Boko Haram yawauwa watu 30 Kaskazini mwa Nigeria

Watu 30 wamepoteza maisha katika mji wa Konduga Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, baada ya magaidi wa kundi la Boko Haram kutekeleza mashambulizi matatu ya bomu.

Shambulizi la Boko Haram
Shambulizi la Boko Haram STEFAN HEUNIS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, mabomu hayo yalilipuliwa na magaidi watatu waliojitoa mhanga na kuwalenga watu waliokuwa wanatazama mechi ya mchezo wa soka kupitia Televisheni katika ukumbi wa michezo.

'Idadi ya watu waliopoteza maisha imefikia 30. Wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa,” amesema Usman Kachalla kiongozi wa operesheni za dharura katika eneo hilo.

Kundi la Boko Haram limeendelea kuwa tishio kwa serikali ya Nigeria tangu mwaka 2002, kupinga serikali ya nchi hiyo kwa madai ya kuendeleza elimu ya Magharibi.

Watu Milioni 2.3 wamekimbia makwao tangu mwaka 2013 huku wengine 250,000 wakikimbilia katika nchi jirani ya Cameroon, Chad na Niger.

Mwaka 2014, kundi hilo liliwateka wasichana 276 wa Shule ya wasichana ya Chibok.

Rais Muhammadu Buahri ameahidi kulimaliza kundi la Boko Haram katika uongozi wake wa muhula wa pili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.