rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Sudani Omar Al Bashir

Imechapishwa • Imehaririwa

Suda: Bashir ashtakiwa kwa makosa ya rushwa

media
Rais wa zamani wa Sudan, Omar al-Bashir. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Mwendesha mashtaka nchini Sudan amemumfungulia mashtaka ya rushwa rais wa zamani wa nchi hiyo Omar al-Bashir.


Bashir ambaye aliondolewa madarakani na jeshi kupitia mapinduzi April 11 baada ya maanadamano ya miezi kadhaa.

Kuangushwa kwake kulimaliza utawala wake uliodumu kwa karibu miaka 30.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan SUNA, Bashir alishtakiwa kwa makosa ya kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha za kigeni nyumbani kwake.

Hata hivyo hakuna taarifa za kina zilizotolewa kuhusu mashtaka hayo.

Al-Bashir ambaye hajaonekana hadharani tangu alipokamatwa, tayari alikuwa amefunguliwa mashtaka mengine ya kuchochea vurugu na kushiriki kujua waandamanaji.

Waendesha mashtaka pia waliagiza Bashir achunguzwe kwa tuhuma za utakatishaj fedha na ugaidi.