Pata taarifa kuu
MALI

Watu zaidi ya 100 wauawa katikati mwa nchi ya Mali

Watu wanaokadiriwa kufikia 100 wameuawa katika mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo katika kijiji kimoja kilichoko katikati mwa nchi ya Mali, tukio hili likiwa ni mfululizo wa machafuko yanayoripotiwa kwenye eneo hilo.

Picha ya moja ya bunduki ambayo hutumiwa sana na makundi ya kimila na yale ya kigaidi nchini Mali
Picha ya moja ya bunduki ambayo hutumiwa sana na makundi ya kimila na yale ya kigaidi nchini Mali PASCAL GUYOT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika katika mauaji haya ambayo yalilenga watu wa jamii ya Dogon, ikionekana ni kama tukio la ulipizaji kisasi ambalo limegharimu maisha ya mamia ya watu.

Shambulio hili limekuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tangu watu zaidi ya 160 kutoka jamii ya Fulani wauawe kwa kuchinjwa na watu waliodaiwa kuwa ni kutoka jamii ya Dogon.

Akiwa nchini Uswis, rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita amesema kamwe nchi yake haiwezi kuwa na mazoea ya ulipizaji visasi ambapo pia akatangaza kukatisha ziara yake.

Rais Keita ametoa wito kwa wananchi wa taifa lake kuungana wakati huu na kukemea vitendo vya ukatili vinavyotekelezwa na jamii zenye uhasama, akisema huu ni wakati wa kuijenga nchi.

Maofisa wa Serikali katika kijiji cha Sobane-Kou ambacho kilivamiwa, wamethibitisha waqtu zaidi ya 95 kuuawa na wengine mamia hawajulikani walipo.

Serikali imetoa idadi ya watu 95 kuuawa na wengine 19 hawajulikani walipo, huku mamia ya mifugo wakichinjwa na nyumba kadhaa kuchomwa moto..

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.