Pata taarifa kuu
LIBYA

UN: Nchi lazima ziongeze muda wa vikwazo vya silaha kwa nchi ya Libya

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyataka mataifa yote duniani kuiwekea vikwazo vya silaha nchi ya Libya, akisema silaha zinazosafirishwa kwa njia ya ardhi, majini na anga zimekuwa zikitumiwa kuchochea machafuko nchini humo.

Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, António Guterres.
Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, António Guterres. SIMON MAINA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu Guterres ametoa wito huu katika taarifa yake kwa baraza la usalama la umoja wa Mataifa, akitaka kukaguliwa kwa meli zote zinazoingia Libya na kuongezwa kwa muda wa vikwazo vya silaha kwa mwaka mmoja zaidi.

Meli ya kivita ya umoja wa Ulaya "Sophia" ndio imekuwa meli pekee ya kijeshi inayofanya operesheni za ukaguzi kwenye bahari ya pwani ya Libya.

Wataalamu wa umoja wa Mataifa ambao wamekuwa wakisimamia makataa ya kuiuzia silaha nchi ya Libya, kwenye ripoti yao wamesema baadhi ya nchi zimeendelea kusafirisha silaha kwenda Libya.

Taarifa ya katibu mkuu Guterres imeongeza kuwa, ili kukabiliana na machafuko yanayoshuhudiwa nchini Libya ni lazima mataifa yakubaliane na kuweka msimamo wa pamoja kuhusu vikwazovya silaha dhidi ya Libya.

Tangu kuangushwa kwa utawala wa Marehemu kanali Moammar Gadhafi mwaka 2011, nchi ya Libya imetumbukia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe makundi mengi yakiwania umiliki wa maeneo yenye utajiri wa mafuta.

Kwa takribani miezi miwili sasa vikosi vinavyoongozwa na mbabe wa kivita nchini Libya Jenerali Khalifa Haftar ambaye ameanzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya utawala wa Tripoli unaotambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.