rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Misri Ugaidi Siasa

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu wenye silaha wawauwa wanajeshi wanane nchini Misri

media
Eneo la sinai nchini Misri Khaled DESOUKI / AFP

Watu wenye silaha, wamewauwa wanajeshi wanane nchini Misri, baada ya kushambuliwa katika kizuizi cha usalama katika eneo la Sinai.


Shambulizi hilo lilitokea katika mji wa El-Arish, wakati watu hao wenye silaha kuanza kuwashambulia wanajeshi hao.

“Wanajeshi wanane wameuawa na watatu kujeruhiwa. Wote walikuwa ni maafisa wa usalama,” alisema afisa wa afya.

Kituo cha Televisheni nchini humo kimeripoti kuwa kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya vifo kuongezeka kwa sababu, mashambulizi hayo yalilenga vituo zaidi.

Shambulizi hili limekuja wakati Waislamu nchini humo wakiadhimisha sikukuu ya Eid al-Fitr.

Hakuna kundi lolote lililodai kutekeleza shambulizi hilo.

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch, limekuwa likisema kuwa maafisa wa usalama wamekuwa wakitekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya raia katika eneo la Sinai, wakati wa kukabiliana na makundi yenye silaha.