Pata taarifa kuu
SUDAN-JESHI-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Jeshi nchini Sudan lafuta makubaliano na waandamanaji na kutangaza Uchaguzi Mkuu

Kiongozi wa Baraza la Kijeshi nchini Sudan Jenerali Abdel Fatta al Burhan, amesema Baraza lake limeamua kufuta makubaliano yote ya awali waliyoafikiana na wakuu wa waandamanaji kuhusu kuundwa kwa serikali ya mpito, na badala yake sasa Uchaguzi Mkuu utafanyika baada ya miezi tisa.

Kiongozi wa Baraza la kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan.
Kiongozi wa Baraza la kijeshi nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan. AFP PHOTO/HO/SUNA
Matangazo ya kibiashara

Awali, wanajeshi ambao ndio waliomundoa madarakani rais wa zamani Omar Al-Bashir mwezi Aprili, walikuwa wamekubaliana na waandamanaji kuunda Baraza la uongozi ambalo lingeongoza serikali kwa miaka mitatau kabla ya kukabidhi rasmi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Tangazo la Jeshi limetolewa wakati huu zaidi ya watu 30 wakiripotiwa kupoteza maisha kutokna na makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama yaliyotokea siku ya Jumatatu, wakati wa operesheni ya kuwaondoa raia katika kambi yao nje ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.

Jenerali al-Burhan amesema makubaliano yote ya awali yamefutwa na sasa uchaguzi Mkuu utafanyika chini ya uangalizi wa Jumuiya za Kikanda.

Ulinzi mkali umewekwa kuzingira makao makuu ya Jeshi baada ya kushuhudia wanausalama waliokuwa na silaha wakiwavamia na kuwalazimisha kuondoa waandamanaji ambapo mamia walijeruhiwa pia..

Marekani na mataifa kadhaa ya barani Ulaya, yamekashifu kile yalichosema ni ukatili dhidi ya waandamanaji, wakati huu mataifa hayo yakiendelea kuweka shinikizo kwa jeshi kukabidhi madaraka.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana siku ya Jumanne kujadili hali inayoendelea kushuhudiwa nchini Sudan.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.