Pata taarifa kuu
CAMEROON-SIASA-UPINZANI-MAANDAMANO

Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon, ashtumu kukamatwa kwa wafuasi wake

Kinara wa upinzani nchini Cameroon Maurice Kamto amekosoa hatua ya vyombo vya usalama nchini humo kuwakamata zaidi ya wafuasi wake 350 walioandamana kushinikiza aachiwe huru.

Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon  Maurice Kamto
Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon Maurice Kamto RFI/Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Kamto ambaye ameendelea kuwa kizuizini tangu mwezi JanuarI, ametoa kauli hii kupitia msemaji wake, akilalama namna vyombo vya usalama vimekuwa vikitumia nguvu kubwa kukabiliana na waandamanaji.

Aidha, amekosoa namna wafuasi wake walivyonyimwa haki ya kupata wanasheria.

Kwa mujibu wa vuguvugu linalomuunga mkono Kamto linalofahamika kama Mouvement pour la renaissance du Cameroun, polisi iliwakamata waandamanaji 350 kwenye mji wa Yaounde na Magharibi mwa mji wa Nkongsamba.

Vuguvugu hilo  limekuwa likiandaa maandamano mfululizo kushinikiza mamlaka nchini humo kumuachia huru  kiongozi wao anayeshtakiwa kwa makosa ya uhaini na kuchochea vurugu mara baada ya Uchaguzi Mkuu.

Kamto sasa anautaka umoja wa Mataifa kuingilia kati kinachoendelea nchini humo na hasa kile alichosema uhalifu unaotekelezwa kwenye eneo ambalo watu wake wanazungumza Kiingereza.

Wanaharakati katika maeneo yanayozungumza lugha ya Kiingereza, wamekuwa wakitaka kujitenga na serikali ya Yaounde na kuunda nchi yao ya Ambazonia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.