Kikosi cha AMISOM kupunguzwa nchini Somalia
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema wanajeshi 1,000 watapunguzwa kutoka kwenye kikosi cha wanajeshi zaidi ya 20,000 wa kulinda amani nchini Somalia maarufu kama AMISOM, licha ya mashambulizi kuongezeka mjini Mogadishu.
Imechapishwa:
Pendekezo hili liliwasilishwa na Uingereza na kuungwa mkono na wajumbe wote katika Baraza hilo lakini ikaamuliwa kuwa kikosi hicho cha AMISOM kitaendelea na operesheni zake nchini Somali kwa mwaka mmoja zaidi.
Hata hivyo, maafisa wa polisi 1,040 kutoka mataifa mbalimbali ya Sierra Leon, Nigeria na Ghana hawatapunguzwa.
Tangu mwaka 2017, kumekuwa na mpango wa kuwapunguza wanajeshi wa AMISOM na taratibu kuanza kukabidhi ulinzi wa nchi hiyo kwa vikosi vya Somalia.
AMISOM iliundwa la Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika mwaka 2007 na kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenda kulinda serikali ya Mogadishu inayotambuliwa kimataifa, lakini pia kuzuia mashambulizi ya kundi la Boko Haram. .
Mataifa ya Afrika yanayounda jeshi la AMISOM ni pamoja na Uganda ambayo ina idadi kubwa ya wanajeshi zaidi ya 6,000 Burundi, Ethiopia, Kenya na Djibouti.
Jeshi la AMISOM, limepiga kambi Kusini na katikati ya nchi hiyo.