Pata taarifa kuu
RIPOTI-WATOTO

Ripoti: Watoto wana hali nzuri leo kuliko miaka 20 iliyopita

Ripoti mpya iliyochapishwa juma hili kuhusu hali ya watoto duniani inaonesha kuwa kuna hatua kubwa imepigwa katika afya, elimu na usalama kwa mataifa mengi katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Watoto wakiwa darasani wakisoma kwenye nchi ya Mali, Save the Children inaitaja mali kutofanya vizuri kwenye ulinzi wa watoto
Watoto wakiwa darasani wakisoma kwenye nchi ya Mali, Save the Children inaitaja mali kutofanya vizuri kwenye ulinzi wa watoto UN Photo/Marco Dormino
Matangazo ya kibiashara

Shirika la kimataifa la Save the Children linasema hali za watoto zimeboreshwa katika nchi 173 kati ya 176, huku Singapore ikiorodheshwa kuwa kinara wa kutoa huduma bora kwa watoto.

Shirika hilo lisilo la kiserikali linakadiria kuwa watoto milioni 690 wamekuwa wakinyimwa haki kutokana na kuumwa, vifo, ndoa za utotoni, mimba za mapema, utapia mlo au kutopata elimu, idadi hii ikiwa ni chini kutoka watoto 970 mwaka 2000.

Nchi za Sierra Leone, Rwanda na Ethiopia zinatajwa kama nchi ambazo kwa kiwango kikubwa zimepiga hatua kuboresha maisha ya watoto katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Kidunia, vifo vya watoto vimepungua na kuna watoto pungufu karibu milioni 49 waliodumaa, huku China na India zikirekodi kiwango cha chini zaidi kidunia.

Katika viashiria 8 vilivyotumiwa na save te Childre kupima maendeleo ya watoto, ni kiashiria kimoja tu ndicho kilichoongezeka, nacho ni ongezeko la idadi ya watoto ambao wamekimbia makwao kutokana na mizozo.

Ripoti inasema watoto milioni 420 wanaishi kwenye ukanda wenye migogoro hii ikiwa ni mara mbili zaidi ya idadi iliyokuwepo mwaka 1995.

Baada ya Singapore, Sweden, Finland, Norway, Slovenia, Ujerumani, Jamhuri ya Ireland, Italia, Korea Kusini na Ubelgiji ziliorodheshwa kama mataifa 10 ambayo watoto wanalindwa zaidi.

Nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati iliorodheshwa kama taifa la mwisho (176) nyuma ya mataifa ya Niger, Chad, Mali, Sudan Kusini, Somalia, Nigeria, Guinea, jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burkina Faso.

Nchi nyingine za Afrika Mashariki ukiondoa Rwanda iliyopiga hatua, Tanzania, Kenya, Uganda na Burundi bado hazifanyi vizuri katika nchi ambazo zinatoa ulinzi wa kutosha kwa watoto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.