Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Waziri Mkuu mpya wa DRC aahidi kuimarisha usalama

Baada ya miezi tano uongozini, rais Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga Ilunkamba kuwa Waziri Mkuu, kuongoza serikali ya muungano kwa mujibu wa makubaliano ya kisiasa kati yake na rais wa zamani Joseph Kabila.

Waziri Mkuu mpya wa DRC Sylvestre Ilunga Ilukamba (Kushoto) akisalimiana na rais Felix Tshisekedi (Kulia) walipokutana jijini Kinshasa Mei 20 2019
Waziri Mkuu mpya wa DRC Sylvestre Ilunga Ilukamba (Kushoto) akisalimiana na rais Felix Tshisekedi (Kulia) walipokutana jijini Kinshasa Mei 20 2019 www.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Ilunkamba ni mshirika wa karibu wa rais wa zamani Kabila na anaanza kazi, akiahidi kuboresha maisha ya wananchi na kurejesha usalama, katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na matatizo makubwa ya kiusalama.

Waziri Mkuu huyu mpya ni mwanasiasa mkongwe nchini DRC, na anatokea katika jimbo la Katanga, na katika uzoefu wake wa kuwa katika ulingo wa kisiasa kwa miaka 30, aliwahi kuwa mshauri wa rais wa zamani Mobutu Seseko.

Kati ya mwaka 1981-1983 alikuwa Naibu Waziri wa Uchumi na baadaye kuwa mshauri wa serikali kuhusu masuala ya uchumi kati ya mwaka 1986-1987 kabla ya kuhudumu baadaye kuwa Waziri wa Fedha.

Uteuzi huu umekuja baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya rais Tshisekedi na Kabila, kwa sababu kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Waziri Mkuu anastahili kutoka kwenye chama chenye wabunge wengi wabunge.

Baada ya Uchaguzi wa wabunge na Magavana, muungano wa FCC ulipata idadi kubwa ya wawakilishi huku muungano wa CACH wa rais Tshisekedi ukishindwa kufikia hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.