Pata taarifa kuu
SUDAN-JESHI-MAANDAMANO-BASHIR-SIASA

Jeshi nchini Sudan lasitisha mazungumzo na waandamanaji baada ya vurugu

Watu 14 wamejeruhiwa kwa risasi nchini Sudan baada ya jeshi kujaribu kuwaondoa waandamanaji waliopiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi jijini Khartoum.

Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan.
Kiongozi wa kijeshi nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan. AFP PHOTO/HO/SUNA
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano haya yameshuhudiwa saa chache baada ya jeshi na viongozi wa waandamanaji kukubaliana kuunda serikali ya mpito itakayodumu kwa muda wa miaka mitatu.

Jeshi kupitia kiongozi wake Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza kusitisha mazungumzo na viongozi wa waandamanaji kwa saa 72, wakati huu waaandamanaji wakiendelea kusisitiza hawataacha kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi.

“Kulikuwa na watu ambao walikuwa na nia mbaya kati ya wanadamanaji waliowalenga maafsa wetu wa usalama,” amesema Jenerali Burhan.

Hata hivyo, waandamanaji wanawalaumu wanajeshi kwa kuwashambulia, kauli ambayo pia imeungwa mkono na Balozi wa Uingereza nchini humo Irfan Siddiq.

Kupitia katika ukurasa wake wa Twitter, Siddiq amesema anasikitishwa kuona jeshi likitumia risasi kuwashambulia waandamanaji.

Kabla ya kusitishwa kwa mazungumzo hayo, wanajeshi na waandamanaji walikuwa wamekubaliana kuunda serikali ya mpito kwa muda wa miaka mitatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.